Wafuasi wa Rais wa Korea Kusini waandamana kupinga kukamatwa kwake
Mamia ya wafuasi wa Rais wa Korea Yoon Suk Yeol walipinga kukamatwa kwake mbele ya ofisi inayochunguza makosa ya ufisadi ya maafisa wa ngazi ya juu katika mji wa Gwacheon Jumatano.
Maafisa wa Korea Kusini Jumatano walimkamata Rais aliyeondolewa na bunge Yoon Suk Yeol kufuatia tuhuma za uasi, huku kiongozi huyo akisema amekubali uchunguzi dhidi yake uendelee ili kuepusha “umwagaji damu”.
Yoon alionekana katika msafara wa magari akiwasili kwenye ofisi ya idara ya kupambana na ufisadi Jumatano asubuhi, ambayo inasimamia uchunguzi huo.
Maafisa wana saa 48 kumuhoji Yoon, baada ya hapo watatafuta hati ya kuendelea kumshikilia kwa siku 20 au kumuachia huru.
Yoon ni rais wa kwanza wa Korea Kusini kukamatwa akiwa madarakani, licha ya kuwa taifa hilo la Asia lina historia ya kuwafungulia mashtaka na kuwafunga jela viongozi wa zamani.
Polisi walikuwa walipeleka maafisa 3,200 kwenye makazi ya Yoon kutekeleza hati ya kumkamata Jumatano, ambako mamia ya waandamanaji wanaomuunga mkono Yoon na wanachama wa chama chake cha People Power walikuwa wamekusanyika kabla ya Alfajiri chini ya baridi kali. - Reuters
#koreakusini #rais #wafuasi #maandamano #ofisiyauchunguzi #ufisadi #voa #voaswahili
5 Jul 2025
- Doctors have credited the 'folds' with playing a crucial role in one's hearing.
5 Jul 2025
- Gachagua said this during her aunt's burial ceremony.
5 Jul 2025
- ODM was responding to The Standard Media's 'Raila's Turf Rebels' article.
6 Jul 2025
- Japan's government on Saturday warned of more possible strong earthquakes in waters southwest of its main islands, but urged the public not to believe unfounded manga comic-book predictions of a major disaster.
6 Jul 2025
- Traders affected by the recent demonstrations held in honour of victims of last year’s anti-Finance Bill protests are now struggling to rebuild their lives and livelihoods.
6 Jul 2025
- Deputy President Kithure Kindiki and other leaders backing the broad-based government have intensified attacks on the opposition, calling for unity to heal the nation.
6 Jul 2025
- The High Commission of Rwanda in Kenya has marked 31 years of liberation — a commemoration of the country’s remarkable transformation, from a painful past under an oppressive regime to a future defined by unity, progress, and resilience.
6 Jul 2025
- Saba Saba's long harvest and why struggle is never wasted
6 Jul 2025
- Joho leads Coast MPs in Ruto campaign
6 Jul 2025
- Mr President you risk bringing idolatry in church, State House
6 Jul 2025
- Kenya today: An angry nation sliding towards self-destruction
6 Jul 2025
- 35 years later, Saba Saba continues: Meeting of different generations, same script
6 Jul 2025
- Parliament's CDF coup: The Senate should halt this constitutional heist