Wahudumu wa afya waanza mgomo baridi Machakos

  • | Citizen TV
    36 views

    Serikali ya kaunti ya Machakos imewaonya wahudumu wa afya ambao wameanza mgomo baridi leo wakitaka kupandishwa vyeo. Kulingana na mkuu wa utumishi wa umma wa kaunti hiyo Albanus Mutisya, kati ya idara kumi za kaunti , wafanyakazi wa sekta ya afya pekee ndio wamekuwa wakipandishwa vyeo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita na kuwataka kuwa na subira