Skip to main content
Skip to main content

Wairimu hakubabaika baada ya Cohen kutoweka, mahakama yaelezwa

  • | Citizen TV
    240 views
    Maafisa zaidi waliochukua taarifa za kutoweka kwa mfanyabiashara Tob Cohen kutoka kwa mkewe Sarah Wairimu wameendelea kutoa ushahidi huku leo mahakama ikiambiwa namna Wairimu hakuonyesha dalili zozote za kubabaika licha ya mumewe kutoweka. Musa Yego, aliyekuwa afisa wa kikosi maalum cha Flying Squad wakati huo, ameelezea mahakama kwamba alimhoji mshukiwa kuhusu ripoti ya kutoweka kwa mumewe, ambaye alimweleza kuwa Cohen alikuwa na mazoea ya kutoka nyumbani kwake na kukosa kurejea kwa siku kadhaa. Hata hivyo, upande wa mshukiwa ulipinga ushahidi wa Yego kwamba haukubaliki katika kesi ya mauaji. Uamuzi wa ombi hilo utatolewa Desemba mosi.