Wakaazi wa Homa Bay wamtaka rais Ruto akamilishe miradi

  • | Citizen TV
    755 views

    Wakaazi wa kaunti ya Homa bay wanamtaka rais William Ruto kuhakikisha kuwa miradi yote iliyoanzishwa na serikali yake imekamilika. wakazi hao wanataka hususan soko la samaki kukamilishwa ili waweze kuendeleza biashara zao kwenye mazingira safi na salama na kujikuza kiuchumi. aidha wakazi hao wanalilia kuimarishwa kwa usalamawakisema kuwa wahalifu wamewakosesha wavuvi amani wanapokuwa ziwani kujitafutia tonge.