Wakaazi wa Kwale wazua tetesi kuhusu uvamizi wa shamba la Kuranze

  • | Citizen TV
    323 views

    Wakaazi wa Kuranze eneo la Kinango kaunti ya Kwale wamezua hofua kufuatia madai kuwa kuna ugawanyaji na uuzaji wa ardhi ya Kuranze kinyume cha sheria. Wakaazi hao wanadai watu binafsi wameanza kupima na kuwauzia watu wasiokuwa na ufahamu vipande vya ardhi hiyo iliyotengewa miradi tofauti ya maendeleo na serikali ya Kaunti ya Kwale. Ardhi hiyo yenye yenye zaidi ya ekari 170,000 imetengewa miradi ya uchimbaji madini, mji wa maonyesho ya madini, ufugaji, ukulima wa kunyunyizia maji na vituo vya biashara.