Skip to main content
Skip to main content

Wakaazi wahimizwa kuchukua hatua za kulinda mazingira Kilifi

  • | Citizen TV
    88 views
    Duration: 2:09
    Wadau wa uhifadhi wa mazingira humu nchini wamekongamana mjini Kilifi ili kujadili mbinu endelevu za kitamaduni za utunzaji wa mazingira hasa maeneo loevu. Wakiongozwa na mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa samaki na viumbe wa majini nchini KMFRI Dkt. Paul Orina, wadau hao wamesema ipo haja kwa jamii kuhamasishwa jinsi ya kutunza maeneo loevu ikizingatiwa kuwa wao ndio wanaoishi katika maeneo hayo. Wakizungumza na wanahabari wadau hao wamedokeza kuwa kando na mabadiliko ya tabia nchi uharibifu mwingi wa maeneo loevu husababishwa na jamii mara nyingi kwa kukosa ufahamu wa kutosha kuhusu jinsi ya kuhifadhi maeneo hayo muhimu.