- 428 viewsDuration: 3:09Shughuli za usafiri zilikatizwa katika barabara ya Ekerore- Nyanchwa huko Bonchari, kaunti ya Kisii baada ya wakazi waliojawa na ghadhabu kufunga barabara hiyo. Wakazi wanalalamikia ubovu wa barabara wakisema mwanakandarasi alifanya kazi duni na kuwasababisha kutafuta njia mbadala ya kupitia kuelekea kisii mjini.na kama anavyoarifu Chrispine, wakazi walilima na kupanda migomba ya ndizi barabarani ili kuonyesha ghadhabu yao.