Skip to main content
Skip to main content

Wakazi wa kijiji cha Sirwa-yala katika kaunti ya Nandi wanaishi kwa hofu kufuatia uvamizi wa kiboko

  • | Citizen TV
    959 views
    Duration: 2:40
    Wakazi wa kijiji cha Sirwa-yala katika kaunti ya Nandi wanaishi kwa hofu kufuatia uvamizi wa kiboko ambaye amekuwa akiharibu mazao yao na kutishia usalama wao. Wakazi hao wanaoishi karibu na kingo za mto Yala wanasema kuwa mnyama huyo hutoka majini nyakati za usiku na kuvamia mashamba yao, akila kila aina ya mazao bila huruma. Wakazi hao sasa wanaiomba serikali kupitia idara husika kuchukua hatua za haraka kumhamisha kiboko huyo na kurejesha hali ya usalama katika eneo hilo.