Wakazi wa Marimanti, Kaunti ya Tharaka Nithi, walipata nafasi ya kujadili masuala ya kilimo, makazi nafuu na usalama wakiwa na maafisa wa kutunga sera kutoka serikali ya kitaifa na ile ya kaunti.
Shughuli hii ilifanyika katika ukumbi wa Kanisa la Methodist Marimanti, ambapo mashabiki wa Muuga FM pia walikutana na watangazaji wao maarufu na kushuhudia matangazo yakipeperushwa mubashara. Muuga FM, kituo cha Royal Media Services kinachoongoza kwa matangazo kwa lugha ya Kimeru, kimeendelea kuwaleta pamoja wasikilizaji na wadau muhimu ili kushughulikia changamoto za kila siku za jamii za Meru na Tharaka Niithi