Wakazi wa Samburu kuruhusiwa kutumia na kuhifadhi misitu ya CFA Krisia

  • | Citizen TV
    485 views

    Katibu wa misitu katika wizara ya mazingira Ephantus Kimotho ameongoza shughuli ya kutia Saini mkataba wa makubaliano kati ya usimamizi wa misitu -KFS na shirika la mpango wa kijamii wa kulinda misitu -CFA katika msitu wa Krisia Kaunti ya Samburu. Mkataba huo unawaruhusu wananchi kutumia msitu huku wakiuhifadhi.