Wakazi wa Wajir kaskazini, waamua kugeukia kilimo ili kujikimu baada ya kupoteza mifugo wengi

  • | K24 Video
    27 views

    Baada ya kupoteza mifugo yao kutokana na ukame na mafuriko, wakazi wengi wa Wajir kaskazini, katika kaunti ya Wajir wameamua kugeukia kilimo ili kujikimu. Wakazi hao wanaamini kuwa kaunti kame ya wajir inaweza kulisha taifa endapo taifa litaweka mbele juhudi za kuvuna maji hasa baada ya kipindi kirefu cha mvua. Ambaye amerejea kutoka kaunti ya Wajir anaangazia juhudi za kilimo zitakazosaidia kaunti ya Wajir kuzalisha chakula.