Wakazi waandamana katika kituo cha afya cha Sosiot

  • | Citizen TV
    434 views

    Majonzi na Hasira zimetanda katika kituo cha matibabu cha sosiot eneo bunge la Belgut kufuatia Kifo cha Mwanamke mmoja. wakazi wa eneo hilo walifanya maandamano wakiibua maswali kuhusu huduma za afya katika kituo hicho ambazo wanadai kuwa duni. familia ya mama huyo inasema kuwa walimpeleka katika kituo hicho asubuhi akilalamikia shinikizo la damu lakini hakupata matibabu kwa zaidi ya saa mbili.aidha wanadai kuwa walikosa huduma ya ambulensi ya kumhamisha kutokana na masuala ya utaratibu.