Mamia ya wakazi katika vijiji vilivyo viungani mwa mji wa Magadi, wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji huku kipindi kirefu cha ukame kikiathiri watu na mifugo. Katika kijiji cha Ol Keri , kilichoko umbali wa kilomita 42 kutoka Magadi, vyanzo vya naji vimekauka baada ya mvua kukosa kunyesha kwa miezi kadhaa. Wakazi sasa wanaitaka serikali irejeshe huduma za maji na kuweka matangi pamoja na mabomba kijijini humo, wakisema hatua hiyo itapunguza masafa marefu wanayotembea kutafuta maji.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive