Shughuli za uchukuzi kwenye barabara kuu ya Maralal - Nyahururu, zimetatizika mchana kutwa katika eneo la Suguta Marmar kaunti ya Samburu, baada ya wananchi kuandamana wakilalamikia vifo vya wanawake wanapojifungua katika hospitali ya Suguta.
Waandamanaji hao waliwasha moto barabarani na kuharibu lango kuu la hospitali hiyo, kabla ya kuliteketeza. Wakazi wanalalamikia utepetevu wa madaktari na usimamizi mbovu wa hospitali. aidha wanadai kuwa wagonjwa huagizwa kununua dawa nje ya hospitali na kulipia ada ya Ambulensi wanapopata dharura.Mwenyekiti wa bodi simamizi ya hospitali hiyo askofu James Lolkurum, amesema kuwa uchunguzi unafanywa.