Wakazi walilia usalama baada ya uhalifu katika kaunti ya Baringo

  • | Citizen TV
    576 views

    Mwakilishi wa kike wa kaunti ya Baringo, Florence Jematia, amemshutumu Inspekta Jenerali wa Polisi kwa kukithiri kwa uhalifu katika kaunti ya Baringo na eneo pana la bonde la ufa. Zaidi ya familia 3,200 wamelazimika kuwa wakimbizi wa ndani kwa ndani kama huku watu 17 wakiuawa mwaka huu. Aidha shule 20 zimefungwa kufuatia ukosefu wa usalama.