Skip to main content
Skip to main content

Wakazi waogopa maafisa wa GSU wanaopiga doria Macalder, Nyatike

  • | Citizen TV
    1,329 views
    Duration: 2:16
    Kituo cha Biashara cha Macalder huko Nyatike kaunti ya migori kimefifia na kuwa kama mahame kutokana na wasiwasi wa utovu wa usalama. Uwepo wa maafisa wa GSU, waliotumwa baada ya wimbi la uhalifu ambalo lilisababisha vifo vya watu watatu na kujeruhiwa kwa wengine wengi wakiwemo maafisa wa polisi, umeongeza hofu. Wakazi wanadai kuwa maafisa hao waliwapiga watu kiholela walipofika siku za kwanza wakati wa kuwasaka wahalifu.