- 2,046 viewsDuration: 3:46Wakazi wa kaunti ya Busia wanaotumia barabara kuu ya kitaifa ya kisumu kwenda Busia wanalalamikia wembamba wa barabara hiyo ambao unachangia ajali za kila mara, waathiriwa wengi wakiwa wahudumu wa bodaboda. Kwa mujibu wa wakazi hao, ajali hizo pakubwa zinahusisha malori ya masafa marefu yanayoelekea mataifa jirani, huku vifo vingi vikiripotiwa.