- 311 viewsDuration: 3:51Muungano wa Wake wa Magavana nchini umetua katika Kaunti ya Pokot Magharibi kwa kampeni kabambe ya kusisimua chanjo dhidi ya saratani ya uzazi. Hatua hii imechukuliwa baada ya takwimu kufichua kuwa ni asilimia nne pekee ya wasichana waliolengwa ambao wamepokea chanjo hiyo, ikilinganishwa na asilimia 79 ya kitaifa. Ziara hiyo inalenga kuongeza mwamko na kuwafikia wasichana wengi zaidi ili kulinda afya zao.