Wakenya 32 wa jamii ya Turkana wameachiliwa huru baada ya kuhukumiwa nchini Uganda

  • | Citizen TV
    2,841 views

    Wakenya 32 wa jamii ya Turkana waliofungwa jela mwaka mmoja na mahakama ya kijeshi nchini uganda sasa wameachiliwa huru na kuruhusiwa kurejea kwao huko urum eneo bunge la loima kaunti ya Turkana. Ndugu jamaa na familia walijitotokeza kuwalaki wapendwa wao waliokuwa wamehukumiwa kifungo cha miaka ishirini gerezani. Na kama anavyoarifu cheboit emmanuel,kulingana na mila tamaduni na desturi ya waturkana,jamaa hao waliofungwa nje ya nchi hawafai kutangamana na familia zao kabla matambiko kufanywa.