Wakulima wa miwa waipa serikali siku tatu kurejesha usagaji miwa

  • | Citizen TV
    1,185 views

    Wakulima wa miwa wametoa makataa ya siku tatu kwa mamlaka ya Kilimo, kubatilisha amri ya kusitisha usagaji wa miwa katika maeneo ya Nyanza na ukanda wa magharibi. Wakizungumza hii leo, wakulima hao pia waliikosoa mamlaka hiyo kwa kutowahusisha katika uamuzi huo huku wakipinga vikali madai ya ukosefu wa miwa katika maeneo hayo.