Wakulima wa parachichi kufurahia mapato zaidi

  • | Citizen TV
    92 views

    Afisa mkuu wa shirika la parachichi nchini Ernest Muthomi ametangaza kwamba wakulima wa parachichi watafurahia bei mpya ya zao hilo katika majuma mawili yajayo. Hali hiyo imetokana na ongezeko la soko ughaibuni. Akizungumza kwenye hafla iliyowashirikisha wadau mbalimbali wa sekta hiyo ya parachichi kaunti ya Nyamira, Muthomi amewashauri wakulima wa parachichi kote nchini kujiunga na vyama vya ushirika ili kuwasaidia kukusanya viwango vya kutosha kwa masoko ya ughaibuni. Afisa huyo amesema wamepata masoko Uchina na India.