Wakulima wasema mimea yao imeharibika kwa sababu ya mbolea ghushi waliotumia

  • | Citizen TV
    112 views

    Baadhi ya wakulima katika eneo bunge la Tinderet kaunti ya Nandi wameitaka serikali kuwapa fidia kutokana na hasara iliyoletwa na mbolea ghushi. Wakulima hao wanateta kuwa mbolea hiyo imeharibu mimea waliyopanda. Wakulima hao kutoka vijiji vya lel Kotet na Maraba wanasema kuwa mahindi waliyopanda imeharibika na kushindwa kunawiri.