Idadi ya waliofariki nchini kutokana na mafuriko kufikia sasa ni watu 188

  • | Citizen TV
    2,417 views

    Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko sasa imefikia watu 188 kote nchini. Haya yanajiri huku watu wanaoishi katika maeneo yenye hatari ya mafuriko na maporomoko ya ardhi wakitaka serikali kuwasaidia kuhamia maeneo salama. Serikali ilitoa makataa kwa wale wanaoishi katika maeneo hatari kuondoka kwa hiari la sivyo watalazimishwa kuondoka. Brenda Wanga anatueleza kuhusu juhudi za wananchi wanaohangaika kutafuta makao mbadala.