- 301 viewsDuration: 2:17Huku maeneo mbali mbali yakiendelea kukabiliwa na baa la njaa humu nchini kutokana na makali ya kiangazi wadau wa kilimo kaunti ya Kilifi wanawashauri wakulima kupanda mimea ambayo inakomaa kwa muda mfupi na pia inayohitaji maji kidogo. Wakiongozwa na mkurugenzi mtendaji wa shirika la Gapeka Children Hope Center Jonathan Guyo , wadau hao wamesema kuwa ipo haja kwa wakulima kukumbatia mbinu za kisasa za ukulima endelevu hasa kwa wale wanaoishi karibu na maeneo Chechepe ikizingatiwa kuwa majira ya mvua yameathiriwa pakubwa na mabadiliko ya tabia nchi.