Walimu 4 wakamatwa kwa tuhuma za wizi wa mitihani Kisii

  • | Citizen TV
    1,838 views

    Polisi katika kaunti ya Kisii wanawazuilia walimu wanne waliokamatwa katika shule ya upili ya Bombaba eneo la Bomachoge Chache baada ya karatasi za mtihani zenye majibu kupatikana mtihani wa KCSE ulipokuwa ukiendelea. Kamanda wa polisi Kisii Charles Kases anasema maafisa wa baraza la mitihani la KNEC waliokuwa wakifanya ziara eneo hilo walinasa karatasi za mtihani wa Jiografia zilizokuwa na majibu mchana wa leo. Kati ya waliokamatwa ni meneja wa kituo hicho Edwin Mokaya, walimu Gideon Omondi, Joseph Nyaosi na Ezekiel Nyambane. Wanne hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani hapo kesho. Hayo yanajiri wakati ambapo wizara ya elimu inashikilia kuwa watafanya jitihada zaidi kuhakikisha kuwa watakaokiuka sheria za mtihani wa kitaifa watakabiliwa kisheria.