Walimu kutoka Kajiado wapinga kupunguzwa kwa marupurupu

  • | Citizen TV
    127 views

    Chama Cha walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri (KUPPET) tawi la Kajiado limepinga vikali pendekezo la mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi kutaka marupurupu ya wafanyikazi wanaohudmu katika mazingira magumu kuondolewa au kupunguzwa. wanasema sehemu nyingi za Kajiado zinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo usafiri, mashambulizi ya wanyamapori, na ukosefu wa maji. aidha wanasema kuwa iwapo fedha hizo zingeondelewa, wanaohudmu katika maeneo hayo watatatizika pakubwa.