Walimu wa Shule za JSS Kaunti ya Nandi wameelezea kutoridhika kwao na Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA), wakidai kuwa mfumo huo mpya umeshindwa kuwapa huduma bora za matibabu ikilinganishwa na bima ya awali. Wakiongozwa na Katibu wa KUPPET Nandi, Stephen Lagat, walimu hao wamesema mpango wa sasa wa SHA una mapungufu makubwa ambayo yanawaacha wengi wao bila msaada wakati wa mahitaji dharura ya kiafya.
Kulingana na Lagat, walimu wamekuwa wakihangaika kupata huduma za kimsingi katika hospitali mbalimbali, hali inayowalazimu kutumia pesa zao kununua dawa na kulipia vipimo.