- 414 viewsDuration: 5:30Walimu wa Shule za sekondari msingi JSS katika Kaunti ya Lamu wamelalamikia mazingira magumu ya kufanyia kazi, huku wakiitaka Serikali kuajiri walimu zaidi. Haya yanajiri huku walimu wa JSS katika kaunti mbalimblali wakiendelea kushinikiza kuwa shule hizo zijisimamie badala ya kuwa chini ya shule za msingi. Kulingana nao, hatua hiyo itaboresha mazingira ya kufundishia na kuhakikisha wanafunzi wanapata huduma bora bila changamoto zinazotokana na migongano ya usimamizi.