Katika jitihada za kupunguza uhaba wa walimu kaunti ya Mandera, eneo bunge la Lafey, hazina ya NG-CDF, imetoa ufadhili kwa wanafunzi 150 wanaojiunga na taaluma ya ualimu katika chuo cha walimu cha Mandera.
Hatua hii inatarajiwa kuziba pengo kubwa lililoachwa na walimu kutoka sehemu zingine za nchi waliotoroka kutokana na tishio la ugaidi ambapo walimu wengi waliopoteza maisha yao.
akizungumza katika chuo hicho cha walimu, mbunge wa Lafey Mohammed Abdi Kheir amesema kupitia mipango kama hiyo itaimarisha viwango vya elimu kaskazini mashariki.