- 1,338 viewsDuration: 3:50Siku moja baada ya Waziri wa Afya Aden Duale, kutangaza kwamba bima ya SHA imeweka mikakati ya kuondoa vikwazo kwa huduma bora za afya kwa walimu, walimu wameandamana huko Nandi. Walimu hao wanadai kuwa licha ya tangazo la waziri, bado wanatakiwa kutoa malipo kutoka mifukoni mwao. Ukaguzi wetu ukibaini kwamba kuna hali ya kutoridhika miongoni mwa baadhi ya walimu nchini, ambao wanaishutumu serikali kwa kubadilisha mpango wa afya uliokuwa unafanya kazi na kuwawekea mfumo mpya usiowafaa.