Walinzi walio tayari kufa kwa ajili ya Papa

  • | BBC Swahili
    18,554 views
    Wengi wanapowaona walinzi wa Vatican, wanaona mavazi ya kupendeza, rangi zinazong'aa na mwendo wa taratibu kana kwamba ni sehemu ya onesho la kihistoria. Kwa macho ya haraka, wanaweza kuonekana kama mapambo ya sherehe au wahusika wa tamthilia ya kifalme. Lakini ukweli uliopo chini ya sare hizo za kuvutia ni wa kushangaza na mzito: hawa ni wanaume waliofundishwa kuua, walio tayari kufa kwa ajili ya Papa. Hawa si walinzi wa kawaida. Ni Swiss Guards – jeshi dogo lenye historia ndefu ya uaminifu, ujasiri, na kiapo cha kujitoa muhanga kwa ajili ya imani na Kanisa. Ukishawajua kwa undani, hutaziona tena picha za Vatican kwa macho yale yale. Mwandishi wa BBC Florian Kaijage amewaangazia walinzi hawa hodari wa Papa. 🎥: @frankmavura #kanisakatoliki #papa ##bbcswahili Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw