- 180 viewsDuration: 3:27Ni afueni kwa wasichana waliotoroka ndoa za mapema katika eneo la Loyangalani kaunti ya Marsabit, hii ni kufuatia hatua ya kupokezwa vifaa vya kuanzisha biashara kama vile ususi na biashara nyinginezo. Pia wasichana hao wameshirikishwa kwenye mpango wa utoaji elimu ya kiufundi katika juhudi za kukomesha mila zilizopitwa na wakati.