Skip to main content
Skip to main content

Wamarekani saba wawekwa karantini Laikipia

  • | Citizen TV
    1,763 views
    Duration: 2:12
    Wafanyakazi saba wa shirika la misaada la Marekani Samaritan's Purse waliokuwa wakihudumu katika juhudi za kudhibiti Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameripotiwa kuhamishiwa katika kituo cha karantini kilichoko katika kambi ya kijeshi eneo la Laikipia. Wafanyakazi hao wanaendelea na karantini ya siku 21 kufuatia masharti mapya ya Marekani kwa raia wanaorejea kutoka DRC. Kufikia sasa, serikali ya Kenya haijatoa taarifa rasmi kuhusu ripoti hizo.