Wanachama wa shamba la Mailwa, Kajiado, wanapinga uchaguzi wa viongozi

  • | Citizen TV
    290 views

    Siku chache baada ya Mahakama ya Kajiado kutupilia mbali kesi iliyowasilishwa kupinga Uchaguzi wa Viongozi wa shamba la Mailwa katika eneo la Kajiado ya Kati, Viongozi wa zamani pamoja na wanachama wanapinga vikali uamuzi huo na kuapa kukata rufaa.Kwa Mujibu wa kundi hilo, Viongozi walioidhinishwa kupitia uamuzi huo wa mahakama wanaandamwa na misururu ya kesi kuhusu madai ya kuwalaghai wanachma vipande vyao vya ardhi. aidha wanasema kuwa uchaguzi uliendeshwa bila kuzingatia sheria.