Shule mbalimbali katika eneo la Mwingi zinaendelea kunufaika na shughuli za upanzi wa miti, katika juhudi za kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti bilioni 15 ifikapo mwaka 2030.
Naibu Kamishna wa Kaunti Ndogo ya Mwingi Kati, Catherine Njoroge, ambaye anaongoza zoezi hilo katika shule tofauti, amesema kila eneo limewekewa malengo maalum na juhudi zinaendelea kuhakikisha yanatimizwa. Waziri wa Kilimo wa Kaunti ya Kitui, Mbaya Kimwele, aliwahimiza wakazi kuendelea kupanda na kutunza miti ya matunda ili kuboresha kuwepo kwa chakula, sambamba na mpango wa kaunti wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.