- 231 viewsDuration: 1:30Wanafunzi wa chuo kikuu cha Bomet wameelezea wasiwasi wao kuhusiana na eneo la kutupa taka lililojengwa na serikali ya kaunti ya Bomet karibu na chuo hicho. Wanasema kuwa eneo hilo linaleta hatari kwa sababu wengi wao wanaishi na kufanya shughuli zao kila siku katika eneo hilo. Hata hivyo,sasa wanaomba idara husika katika uongozi wa kaunti ya Bomet ihamishe eneo hilo la kutupa taka hadi eneo jingine kwa sababu pia imekaribiana na mto Nyangores ambao unasambaza maji kwa mji mzima wa Bomet na maeneo mengine.