Wanafunzi wa kike waliofanya mitihani wa kitaifa ya KCPE na KCSE katika eneo la Likoni wahamasishwa

  • | Citizen TV
    117 views

    Wanafunzi wa kike waliofanya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane (KCPE) na wa kidato cha nne (KCSE) eneo la Likoni kaunti ya Mombasa wamehamasishwa kuhusu mbinu za kukabiliana na changamoto za maisha kipindi hiki cha likizo. Wasichana hao wameelimishwa jinsi watakavyoepuka kujiingiza kwenye vitendo vitakavyowasababishia mimba za utotoni na utumizi wa mihadarati.