Skip to main content
Skip to main content

Wanafunzi watakaojiunga na gredi 10 wana fursa nyingine ya kutuma barua za kurejelewa kwa maombi yao

  • | KBC Video
    320 views
    Duration: 2:09
    Wanafunzi ambao wangali wanatafuta usaidizi kuhusiana na suala la kujiunga na gredi ya 10 wana fursa nyingine ya kutuma barua za kurejelewa kwa maombi yao baina ya tarehe 6 na 9 mwezi Januari mwaka 2026. Kwa mujibu wa waziri wa elimu Julius Migos, maombi yaliyokosa kuidhinishwa yalihusishwa pakubwa na kutojumuishwa kwa masomo hitajika au kutokuwa na uwezo wa kuwapokea wanafunzi katika shule walizochagua. Wizara ya elimu ilipokea malalamishi 355,457 ili kuyarejelea huku kila mwanafunzi akiruhusiwa kutuma maombi manne. Jumla ya wanafunzi 211, 636 walipokea idhinisho ya kurejelewa kwa maombi yao. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive