Wanahabari kadhaa wajeruhiwa wakati wa msako wa uvutaji shisha unaoendelezwa na NACADA

  • | KBC Video
    66 views

    Wanahabari kadhaa kutoka mashirika tofauti ya habari walijeruhiwa jana usiku, baada ya kuvamiwa na walinzi wa klabu wakati wa msako wa uvutaji Shisha unaoendelezwa na halmashauri ya kitaifa ya kukabiliana na uraibu wa pombe na mihadarati, NACADA katika eneo la burudani la Kettle House Bar and Grill mtaani Lavington Muthangari, kaunti ya Nairobi. Baadhi ya wale waliojeruhiwa ni pamoja na mpiga picha wa shirika la utangazaji KBC Jane Kibira na maafisa kadhaa wa polisi. Afisa wa halmashauri hiyo anayeongoza msako huo Nicholas Kosgei amelaani vikali kisa hicho, akisema kwamba hawatalegeza kamba katika vita vya kukabiliana na dawa za kulevya. Muungano wa wanahabari humu nchini umekashifu tukio hilo huku ukitaka wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive