Wanajeshi wa KDF wanaaminika kuuwawa baada ya gari lao kukanyaga kilipuzi Lamu

  • | Citizen TV
    4,252 views

    Taharuki imetanda katika kaunti ya Lamu kufuatia shambulio la kigaidi dhidi ya wanajeshi wa KDF. Inaaminika kuwa wanajeshi kadhaa wa KDF walifariki baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kukanyaga kilipuzi cha kutegwa ardhini kati ya eneo la Milimani na Basuba wadi ya Basuba kaunti ya Lamu. Inaarifiwa kuwa wanajeshi hao walikuwa wametoka kambi yao ya Baure wakisafiri kuelekea kuchukua ngombe eneo la Milimani ambapo walikutana na maafisa wa polisi wa akiba na GSU wakiwaletea mifugo hao. Gari lao lilikanyaga kilipuzi cha ardhini kinachoaminika kutegwa na magaidi wa Alshabab walipokuwa wakirudi kambini. waliojeruhiwa wanapoke amatibabu katika hospitali ya kambi ya Manda.