Wanakandarasi wanaohudumu Teso Kaskazini waonywa dhidi ya uzembe na utepetevu

  • | Citizen TV
    589 views

    Wanakandarasi wanaohudumu katika eneo bunge la Teso Kaskazini kaunti ya Busia wameonywa dhidi ya uzembe na kufanya kazi isiyofikia viwango haswa katika ujenzi wa madarasa kuwa watachukuliwa hatua. Haya yanajiri huku bodi ya kitaifa ya NG-CDF ikitoa changamoto kwa wabunge kote nchini kuwekeza pakubwa kwa kutekeleza miradi ambayo itatoa fursa kwa wananchi kupata ujuzi wa kuwawezesha kujisimamia kimaisha.