Wanakandarasi wazembe waonywa na serikali ya kaunti ya Samburu

  • | Citizen TV
    110 views

    Gavana wa Samburu Lati Lelelit amewaonya wanakandarasi wazembe wanaotekeleza kazi duni kuwa chuma chao ki motoni. Gavana Lati amesema kamwe hatoruhusu fedha za umma kufujwa kupitia utendakazi duni wa wanakandarasi. Hayo yamejiri wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa maji wa gharama ya shilingi milioni hamsini eneo la Sesia Samburu Mashariki. Mradi huo umefadhiliwa na serikali kuu na Ile ya Kaunti.