Wanamazingira wafanya maandamano jijini Nairobi

  • | K24 Video
    128 views

    Tukiendelea na masuala ya mazingira, wanaharakati wanazitaka nchi zilizostawi kutoa fedha walizoahidi wakati wa mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi wa cop 15. fedha hizo za kila mwaka ambazo ni billioni mia moja dola za marekani, zilipaswa kuwa kama fidia kwa mataifa yanayokabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi licha ya kuwa hayajachangia uharibifu wa mazingira. Fedha zilipangiwa kutumika katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya anga kama kiangazi cha muda mrefu na mafuriko.