‘Asilimia 30 ya Wanariadha wa kike kaunti ya Elgeyo Marakwet wameweza kupitia changamoto za dhulma za kijinsia’ Haya ni kwa mujibu wa Waziri anayesimamia maswala jinsia na utamaduni nchini Anne Cheptumo .
Kulingana naye, visa hivyo vingi vinatoka kwa watu wa karibu wa familia ,jambo ambalo amesema kuwa yafaa jamii kushirikiana ili kuangamiza jinamizi hilo. Akizungumza mjini Iten Alipowatembelea wanariadha kambini, Cheptumo amewashauri wanariadha kuripoti visa hivyo ili hatua mwafaka zichukuliwe kwa wakati unaofaa.