Wanawake kunufaika na mpango wa chuo kikuu cha Nairobi wa kuwawezesha kiuchumi

  • | KBC Video
    32 views

    Wanawake zaidi wanatarajia kufaidika na mpango wa chuo kikuu cha Nairobi cha kuwawezesha wanawake kiuchumi, mpango unaodhamiria kuwawezesha wanawake wafanyibiashara kuongeza thamani kwa bidhaa zao kupitia kuimarisha uwezo wao. Akiongea wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya siku tano yaliyoandaliwa katika taasisi ya utafiti na maendeleo ya viwanda hapa Nairobi, Prof Margaret Kobia kutoka kituo cha mafunzo kuhusu wanawake wa Afrika katika chuo kikuu cha Nairobi alitoa wito kwa wanawake kutumia ujuzi waliopata kupitia mafunzo hayo kujikimu na kukabiliana na umaskini.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channell: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #womenempowerment #dirayamagwiji