Wandani wa Rais Ruto kaunti ya Nyeri watetea utendakazi wa serikali

  • | Citizen TV
    253 views

    Kinyume na awali ambapo walikosa kurejea mashinani kwa kushiriki kumng’atua aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua afisini, Wandani wa Rais William Ruto katika kaunti ya Nyeri wameonekana kurejea mashinani kwa kishindo, kutetea sera za serikali ya Kenya Kwanza. Wakiongozwa na katibu katika wizara ya Kawi Alex Wachira, Viongozi hao ambao wameanzisha vikao vya Faragha na wakaazi wa kaunti hiyo, wamewataka wakazi kutoshurutishwa kujitenga na serikali, ila wajitahidi kuiunga serikali mkono kwa manufaa yao.Juhudi hizo zinazoonekana kupata kasi baada ya ziara ya Rais William Ruto eneo la kati majuma matatu yaliyopita, zinanogeshwa huku akitarajiwa tena eneo hili mwezi wa nane.