Baada ya kubwagwa kwenye uchaguzi Mdogo wa Olkalou, Wandani wa Rais William Ruto sasa wameutaka upinzani kujiandaa kwa kinyanganyiro Kizito kwenye uchaguzi mkuu wa Mwaka Ujao. Wakizungumza katika kampeni za kuipigia serikali debe kwenye kaunti za Bungoma,Vihiga, Uasin Gishu, Siaya na Migori, viongozi hao wamerai upinzani kukubali matokeo ya uchaguzi wa mwaka ujao, kama wao walivyokubali kushindwa alhamisi. Aidha wameonya mrengo huo dhidi ya kuendelea kueneza siasa za chuki na migawanyiko, wakiwaomba wakenya kumpa Rais Ruto muhula wa pili wa uongozi ili kumuezesha kukamilisha ajenda yake ya maendeleo.