Skip to main content
Skip to main content

Wanunuzi wa kahawa watakiwa kuwalipa wakulima chini ya siku tano

  • | KBC Video
    62 views
    Duration: 4:42
    MAGEUZI SEKTA YA KAHAWA Rais William Ruto amewaagiza wanunuzi wa kahawa kuwalipa wakulima katika muda wa siku tano baada ya wao kuwasilisha mazao yao. Kiongozi wa taifa amesema malipo ya haraka ni miongoni mwa mageuzi kadhaa yanayonuiwa kufufua sekta ya kahawa. Kiongozi wa taifa ambaye aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mpango maalum wa ufufuzi wa zao la kahawa huko Kianyaga, kaunti ya Kirinyaga alisema mageuzi hayo pia yatajumuisha kutengwa kwa mgao wa shilingi bilioni-2 katika kipindi kijacho cha kifedha katika hatua inayonuiwa kugharamia madeni ya tangu jadi ambayo wakulima wa kahawa pamoja na vyama vya ushirika vinadaiwa. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive