WASHINGTON BUREAU - TAHARUKI BUNGENI MAREKANI BAADA YA SPIKA KUONDOLEWA

  • | VOA Swahili
    994 views
    Wiki hii tunaangazia baraza la wawakilishi la Marekani ambalo limejikuta kwenye hali tete, na huenda lisiwe na kiongozi kwa takriban wiki moja kufuatia kuondolewa kwa spika Kevin McCarthy. Hii ni hatua ya kihistoria ambapo hali hii ilijiri baada ya warepablikan walioasi kupiga kura kumuondoa katika wadhifa wake. Je hatua hiyo itakiathiri chama cha Republikan au hata siasa za Marekani kwa ujumla? #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.