Watangazaji wa Radio Citizen wajumuika na waumini wa kanisa la Jetview SDA

  • | Citizen TV
    148 views

    Katika juhudi za kushirikiana najamii, Kikosi cha Radio Citizen kilijumuika na waumini katika Kanisa la Jetview SDA mtaani Utawala, jijini Nairobi ambapo watangazaji walitoa shukrani zao kwa mashabiki wa stesheni hiyo ya redio inayomilikiwa na kampuni ya Royal media services. Aidha kikosi hicho kiliwahimiza viongozi wa kanisa kuendelea kuwakuza na kuwaelekeza vijana kimaadili ili kujenga kuwa kizazi bora cha hapo baadaye. Hafla hiyo ni mojawapo ya juhudi za redio citizen za kuimarisha uhusiano na jamii na kuhamasisha ushirikiano.